Ad: tangaza na sammisago.com - sammisago@yahoo.com Ads Separator

Entertainment

Lil Twist anazidi kufata nyayo za Lil Wayne,ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela,

By  | 

Rapa wa Young Money Lil Twist amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kama athabu ya tukio alilofanya mwaka 2014.

Lil Twist alivunja nyumba ya Mwigizaji Chris Massey na kuiba saa ya thamani kubwa aina ya Rolex baada ya kumpiga vibaya mwigizaji huyo.

Lil Twist alijisalimisha kwa polisi mwaka huu mwezi wa tisa na kukubali athabu hio kama njia ya kukwepa hukumu kubwa zaidi ambayo ingekuwa miaka 10 jela.

Lil Wayne amekuwa akimtetea staa huyu kwenye matukio tofauti hata pale meneja wa Justin Bieber aliposema kuwa Lil Twist alikuwa akimfundisha tabia mbaya msanii wake. Twist ataanza kutumikia athabu hio Feb. 3 na labda kutoka August 2017.

PATA STORI KIRAHISI ZAIDI,BONYEZA HAPA KUIPATA SAMMISAGO.COM KWENYE >INSTAGRAM >FACEBOOK > TWITTER

Comments