Ad: tangaza na sammisago.com - sammisago@yahoo.com Ads Separator

Entertainment

Mwana FA amewataja wasanii wa Hip Hop wa bongo anaowakubali…

By  | 

Msanii wa Hip Hop Tanzania Hamisi Mwinjuma a.k.a Mwana Fa ameweka wazi kuwa Professor Jay na Marehemu Albert Mangwea ndio wasanii wake bora wa hip hop wa muda wote kwa hapa Bongo.

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live Cha East Africa,FA ametanabaisha kuwa Proffesor ndiye msanii aliyewahi kumpa yeye changamoto za kufanya kazi bora zaidi na kuongeza kuwa Professor ndiye ameleta heshima kwenye muziki wa hip hop bongo.

Kwangu mimi MC wangu bora wa siku zote ni Professor Jay, wasanii wangu bora wawili wa era zote za hip hop ya bongo ni Professor Jay na Marehemu Mangwea..Proffessor Jay ndiye mtu aliyefanya huu muziki uheshimiwe,baada ya Chemsha Bongo kila kitu kilibadirika” alisema Mwana FA.

PATA STORI KIRAHISI ZAIDI,SAMMISAGO.COM IPO INSTAGRAM>INSTAGRAM

Comments