Ad: tangaza na sammisago.com - sammisago@yahoo.com Ads Separator

Entertainment

Mwana FA alivyoiponda hii kauli ‘Eti msanii akioa hawezi kufanya hit song’..

By  | 

Msanii wa wa hip hop Tanzania ,Mwana Fa ambaye mwezi mmoja uliopita alifunga ndoa amefunguka na kusema kuwa hatua ya yeye kuoa haiwezi kumfanya apotee kwenye muziki.

Kupitia FNL na @sammisago Mwana FA amesema atawa ‘Prove Wrong‘ watu wote wanaoamini ndoa zinawafelisha wasanii kwenye muziki kwani ana ngoma ambayo anataka kuiachia ambayo anajua lazima itakuwa hit song.

Mwana FA alisema “Ile kauli kwamba ukioa hufanyi hit song,embu tuone sasa,wasubiri ngoma yangu inayofuata halafu ikishatoka waje tena waulize hilo swali, mimi nina ngoma kali ile mbaya na najua nikiitoa itavuma,nafikiri nitakuwa mbadilishaji wa hiyo mentality“.

PATA STORI KIRAHISI ZAIDI,SAMMISAGO.COM IPO INSTAGRAM>INSTAGRAM

 

Comments