Ad: tangaza na sammisago.com - sammisago@yahoo.com Ads Separator

Entertainment

T.I. amtetea mtoto wake aliyekamatwa na silaha kwenye kiwanja cha ndege.

By  | 

Rapper T.I. anamtita mtoto wake wa kufikia aliyekamatwa akitembea na silaha kinyume na sheria. Zonnique Pullins  ni mtoto wa mke wa T.I aliyempata kabla hajakutana na T.I na amelelewa na T.I.

Hivi karibuni Zonnique alikamatw na silaha aina ya Pisto 38 Caliber na ilichukuliwa na askari kwenye kiwanja cha ndege baada ya mtoto huyu kushindwa kuonyesha kibali cha silaha hio.

Watu karibu na T.I wanasema Zonnique alikuwa kwenye kiwanja hicho cha ndege akienda kumuona mpenzi wake na alichukua pochi ambaye hakuwa na ampango wa kusafiri nayo ila alipofika kwenye uwanja wa ndege ndipo alipogundua na hakujua kama palikuwa na silaha.

Watu wengine wanasema walimsikia T.I akisema ni haki ya mtoto wake kujilinda na kutembea na silaha.

Mtoto huyu alinunua silaha baada ya kukutana na vitisho kwenye mitandao ya kijamii na kwamba alibidi awe na silaha ya kujilinda muda wote sababu baba yake ni mtu maarufu.

ti 2 ti

#StoriByJoeFahamu

Pata Stori Kirahisi Zaidi,Sammisago.Com Ipo Instagram>INSTAGRAM

Comments